Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MABANDA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum la polisi wanawake kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akiongozana na Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Alhaji Omari Mahita (kulia), kuelekea kukagua mabanda wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akisikiliza maelezo ya jinsi silaha inavyohakikiwa   kutoka kwa Afisa wa Jeshi la Polisi,   Kitengo cha Udhibiti wa Silaha, Dotto Shilogile, alipotembelea mabanda ya maonesho wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akiangalia silaha ambayo imeshahakikiwa, alipotembelea banda la Kitengo cha Ukaguzi wa silaha wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Wapili kushoto ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akisikiliza maelezo ya uendeshaji salama wa vyombo vya moto kutoka kwa Koplo Nduguru, alipotembelea banda la askari wa usalama barabarani, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akizindua kitabu kinachoeleza Historia ya Miaka 10 tangu kuanzishwa Mtandao wa Polisi Wanawake wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya mtandao huo, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, Kamishna Alice Mapunda. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani (wapili kulia),  akimkabidhi cheti mmoja wa askari mstaafu alietoa mchango wake wakati wa uanzishwaji wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania , wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya mtandao huo, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Kulia ni Kaimu  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Mussa Ali Mussa. 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Anayeshuhudia kushoto ni Kaimu   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Mussa Ali Mussa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.