Habari za Punde

MAMENEJA TEMESA WAHITIMU MAFUNZO USIMAMIZI WA MANUNUZI NA MIKATABA

 Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (katikati) akitoa msisitizo wakati alipokua akizungumza na Mameneja na wakuu wa vituo kutoka wakala huo (hawapo pichani) kabla ya kuwatunuku vyeti baada ya kumaliza mafunzo ya Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba yaliyomalizika mwishoni mwa wiki, Kulia ni  Mhandisi Dkt Ramadhan Mlinga aliyeendesha mafunzo hayo na kushoto ni Mhandisi Aurelia Ngopa kutoka Temesa. Mafunzo hayo yalifanyika katika chuo cha Uhandisi na Teknolojia (COET) Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 Baadhi ya Mameneja na wakuu wa vituo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Mhandisi Aurelia Ngopa alipokua akisoma risala kwa mgeni rasmi wakati wa sherehe ya kuwatunuku vyeti Mameneja hao baada ya kuhitimu mafunzo ya Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo cha Uhandisi na Teknolojia (COET) Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 Baadhi ya Mameneja na wakuu wa vituo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza mgeni rasmi Mhandisi Japhet Maselle alipokua akizungumza nao wakati wa sherehe ya kuwatunuku vyeti Mameneja hao baada ya kuhitimu mafunzo ya Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo cha Uhandisi na Teknolojia( COET) Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle katikati akifurahia jambo na Mkuu wa kivuko Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe wakati akimkabidhi cheti chake baada ya kumaliza mafunzo ya Manunuzi na Usimamizi wa Mikataba yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika chuo cha Uhandisi na Teknolojia (COET) Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Mhandisi Aurelia Ngopa na kulia kwa mkurugenzi ni Mhandisi Dkt Ramadhan Mlinga.
Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle katikati (aliyevaa suti) akiwa katika picha ya pamoja na mameneja  na wakuu wa vituo kutoka wakala huo mara baada ya kuwatunuku vyeti baada ya kumaliza Mafunzo ya Manunuzi na usimamizi wa mikataba katika sherehe zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo cha Uhandisi na Teknolojia( COET) Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.