Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA MTANANGE WA SIMBA VS LIPULI JANA

Beki wa Lipuli Fc, Asante Kwasi (wa tatu kushoto) akiruka kuwania mpira na mshambuliaji wa Simba, John Bocco, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1 huku Simba wakiwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kiungo wake Mwinyi Kazimoto katika dakika ya 15 na Lipuli wakasawazisha dakika ya 20 kupita kwa beki wao Asante Kwasi kwa mpira wa adhabu ndogo. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Beki wa Lipuli Fc, Joseph Owino (kushoto) akiwania mpira na Mshambuliaji wa Simba John Bocco, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.
 Hussein wa Lipuli akichuana na Niyonzima
 Niyonzima akijiandaa kupiga shuti huku akizongwa na Joseph Owino (kushoto)

  Bocco akifunga bao lililokataliwa kwa kuotea
 Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, akijaribu kumtoka beki wa Lipuli Fc, Hussein Rashid, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

 Simba wakishangilia bao lao lililofungwa na Mwinyi Kazimoto dakika ya 15 kipindi cha kwanza.

Lipuli wakishangilia bao lao lililofungwa na Asante Kwasi dakika ya 20 kipindi cha kwanza.
 Kipa wa Lipuli Fc, Agathon Mkwando, akiruka kuokoa hatari langoni kwake dhidi ya Simba wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.
 Beki wa Simba, Mohamed Hussein (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa Lipuli, Hussein Rashid, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, jana.
 Winga wa lipuli Fc, Seif Rashid, (wa pili kushoto) akijaribu kuwatoka wachezaji wa Simba, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, jana.
 Seif Rashid wa Lipuli Fc, (kushoto) akichuana kuwania mpira na Muzamiru Yassin wa Simba wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana. 
 Shaban Ada (kulia) akichuana kuwania mpira na Jonas Mkude...
  Kichuya akijaribu kumtoka beki wa Lipuli.... 
 Shaban Ada akijaribu kumdhibiti Erasto Nyoni....
 Kiungo wa Lipuli Shaban Ada akihojiwa na waandishi wa habari.
 Viongozi wa Lipuli wakishangilia baada ya kupulizwa filimbi ya mwisho kuashiria kumalizika kwa mchezo huo na kupata droo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.