Habari za Punde

MBUNGE WA MULEBA KUSINI CCM ANNA TIBAIJUKA ATANGAZA KUACHANA NA JIMBO LAKE UCHAGUZI UJAO

Mbunge wa Muleba Kusini kupitia CCM, Prof. Anna Tibaijuka, ametangaza kung’atuka nafasi ya ubunge kwa kutogombea tena kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.
Mheshimiwa Tibaijuka alitangaza uamuzi huo walipokuwa wakizungumzia miaka miwili ya Rais John Pombe Magufuli tangu aingie madarakani ambaye alikuwa kwenye ziara mkoani Kagera.
"Sisi ni watu wazima, kizazi chetu tumeshamaliza kazi tumeshastaafu, na mimi nikimaliza ubunge muhula huu nastaafu nakwenda Muleba, na kuaga nimeshaaga wananchi wameniamini, napenda tuwape nafasi vijana washike nchi", amesema Mama Tibaijuka.

Mama Tibaijuka amekuwa mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 2010, na alishawahi kukumbwa na kashfa kubwa ya pesa za Escrow na kumfanya aondolewe katika nafasi ya Uwaziri katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.