Habari za Punde

MKAZI WA IRINGA AIBUKA NA KITITA CHA MILIONI 161 YA M-BET

 Ofisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (katikati) akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. Milioni 161, mshindi wa mchezo wa Perfect 12, Alex Kalinga (kulia) aliyejishindia katika bahati nasibu ya M-Bet. Kushoto ni Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai. 
Mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Alex Kalinga 'akipozi' na mfano wa hundi mara baada ya kukabiziwa
*******************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Mkazi wa Iringa, Alex Kalinga (26) amejishindia kitita cha sh milioni 161 kwa kubashiri kwa usahihi mchezo maarufu kwa ‘Perfect 12’ unaondeshwa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya M-Bet.
Kalinga alikabidhiwa kitita chake jana na Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley kwa kushirikiana na Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai.
Malley alisema kuwa Kalinga alifanikiwa kubashiri sahihi jumla ya mechi 12 kati ya 17 na kuwa mshindi wao wa droo ya 17 tokea kuanzishwa kwa mchezo wa Perfect 12.
Alisema kuwa  serikali imejipatia jumla ya Sh milioni 29 kutoka kiasi hicho cha fedha ambacho ni asilimia 18 kwa mujibu wa sheria.
“Ni faraja kubwa kuona kijana mwenye umri wa miaka 26 akishinda mamilioni  ya fedha kwa kutumia kiasi cha She elfu moja  tu, hii imedhihirisha kuwa M-Bet ni nyumba ya mabingwa, tunawaomba mashabiki wa soka kuendelea kucheza mchezo wetu ili kujishindia fedha,” alisema Malley.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Kalinga alisema kuwa hakuamini taarifa ya kushinda mchezo huo mara baada ya kupokea simu ya kujulishwa kushinda.
“Nina furaha sana, mimi ni fundi wa kuchomelea mageti ya chuma, sikuwa na kipato kikubwa pale Iringia Mjini, nitaanza kujenga nyumba na kufungua kiwanda cha kuchomelea na nyingine kusaidia familia yangu,” alisema Kalinga.
Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Catherine Lamwai aliwashukuru M-Bet kwa kuendelea vyema na shughuli zake mbali ya kuwazawadia washindi mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.