Habari za Punde

NAPE NNAUYE AWEKA WAZI MSIMAMO WAKE WA KUHAMA AMA KUBAKI CCM

Nape kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter amepost picha ambayo wako watatu akiwemo yeye, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, na aliyekuwa Mbunge wa Singida kupitia CCM ambaye amejivua uanachama , Lazaro Nyalandu.
Baada ya kuweka picha hiyo Mh. Nnauye ameandika maneno ambayo yanaonesha hana mpango kabisa wa kuhama chama chake kama ambavyo inahisiwa na watu mbali mbali.
“Chama cha siasa ni itikadi, itikadi ni imani. Siamini sana katika kubadili imani kienyeji. Nitashughulikia mapungufu nikiwa ndani na sio nje!” Ameandika Nape
Kufuatia Mh Nape Nnauye kuonesha msimamo wake huo, hatua hii moja kwa moja itafunga majadiliano ya watu katika sehemu tofauti kuwa ana mpango wa kukitosa chama cha CCM.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.