Habari za Punde

SERIKALI YA TANZANIA YASAINI MKATABA WA SH. BILIONI 75 NA SERIKALI YA FINLAND

 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kulia) akisaniana mkataba wa makubaliano ya msaada wa Sh. Bilioni 75 na Balozi wa Finland nchini Tanzania, Pekka Hukaa, kwa ajili ya kuisaidia Tanzania katika upatikanaji wa maendeleo endelevu. Hafla hiyo fundi ya kutiliana saini ilifanyika Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO) 
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kulia) akibadilishana mkataba wa makubaliano ya msaada wa Sh. Bilioni 75 na Balozi wa Finland nchini Tanzania, Pekka Hukka, baada ya kutiliana saini kwa ajili ya kuisaidia Tanzania katika upatikanaji wa maendeleo endelevu. Hafla hiyo funpi ya kutiliana saini ilifanyika Ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.
HAFLA YA UTIAJI SAINI MIKATABA MITATU YA MISAADA KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA FINLAND

Napenda kutumia fursa hii kuwajulisha kwamba, leo tarehe 29 Novemba, 2017 tumesaini mikataba mitatu ya Msaada toka Serikali ya Finland. Kwa upande wa Serikali ya Tanzania, mikataba imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango. Aidha, kwa upande wa Serikali ya Finland mikataba hiyo imesainiwa na Mheshimiwa Balozi wa Finland nchini Bw. Pekka Hukka.
  1. Kupitia makubaliano haya, Serikali ya Finland itaipatia Serikali ya Tanzania Euro 28.8 milioni, sawa na Shilingi 75 bilioni. Fedha hizi ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ifuatayo:
  2. i)                   Taasisi ya Uongozi (Euro 9.90 milioni),
Mradi huu unalenga kusaidia upatikanaji wa maendeleo endelevu na kuondoa umasikini nchini na Afrika kwa kuimarisha uwezo wa viongozi na kufanya maamuzi sahihi yenye tija kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa.
ii)                 Mfumo wa kuimarisha Ubunifu nchini (Euro 8.95 million),
Mradi unalenga kuiimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wabunifu kuweza kubuni na kuendeleza ubunifu wao ili kuchochea ukuaji wa viwanda. Kupitia mradi huu wabunifu watasaidiwa kwa njia tatu: moja, Watu wenye ubunifu watapatiwa vifaa na Msaada wa kitaalamu kuyaendeleza mawazo yao ili wayafanye ya kibiashara. Lengo ni kubadili mawazo hao kuwa viwanda. Pili; Watu kutoka taaluma mbalimbali wataunganishwa waweze kutatua changamoto katika viwanda vilivyopo nchini ili vifanye kazi kwa ufanisi, na Tatu; Wabunifu wachanga, Wataalamu vyuoni, Wataalamu Serikalini na Sekta binafsi watapata nafasi ya kutembelea Finland na kujifunza kutoka kwa wenzao namna ya kuendeleza ubunifu. 
iii)               Programu ya misitu (Euro 9.95 million)
Mradi unalenga utuzaji wa misitu na uongezaji thamani ya mazao yatokanayo na misitu kwa lengo la kuongeza kipato kwa Wananchi, kupunguza umasikini na kulinda mazingira.
  1. Hii sio mara ya kwanza kwa  Serikali ya Finland kuunga mkono shughuli za maendeleo ya Serikali. Baadhi ya miradi ambayo Tanzania imenufaika ni pamoja na:
  2. i)                   Mradi wa kilimo biashara Mkoani Lindi na Mtwara (LIMAS), Euro milioni 9,
  3. ii)                 Mradi wa kuimarisha usambazaji na upatikanaji wa umeme wa uhakika Jijini Dar es Salaam, Euro milioni 25, na
iii)              Programu ya maboresho ya Serikali za Mitaa, Euro milioni 10.5
  1. Kwa mara nyingine tena, napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mhe. Balozi wa Finland nchini Bw. Pekka Hukka kwa Msaada aliotupatia. Vile vile, kwa niaba ya Serikali napenda kumuahidi kuwa, Msaada uliotolewa utatumika katika malengo yaliyokusudiwa.
  2. Nashukuru kwa kunisikiliza.
BW. DOTO M. JAMES
KATIBU MKUU
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
NOVEMBA, 2017
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.