Habari za Punde

SHAMTE NA WENZAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI WASOMEWA MASHITAKA SITA LIKIWEMO LA UTAKATISHAJI


 Wakili maarufu nchini, Dkt. Ringo Tenga, Mfanyabiashara Peter Noni, Wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar esSalaam, leo na kusomewa mashitaka yanayowakabili.
Walioshitakiwa ni pamoja na Dkt. Ringo na wenzake pamoja na Wakurugenzi wa Kampuni ya Six Telecom, Hafidh Shamte, Ofisa fedha wa kampuni hiyo, Noel Chacha.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka Sita ya kufanya udanganyifu, kukwepa kulipa ada kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kutakatisha zaidi ya Dola za Kimarekani milioni tatu.
Washitakiwa hao wamesomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Victor Nongwa.  
Washitakiwa hao wakipanda ngazi kuelekea Mahakamani kusomewa mashitaka yao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.