Habari za Punde

SWAHILI FASHION KURINDIMA DESEMBA 1,2,3*********************************************************************************

NA MWANDISHI WETU
MIAKA kumi ya Onyesho la mitindo la Swahili Fashion inatarajia kufanyika Desemba 1, 2 na 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Lengo la tamasha hilo ni kuadhimisha miaka kumi ya utamaduni wa mswahili ambapo limekuwa likifanyika kila mwaka tangu 2008.
Onyesho hilo linatarajiwa kupambwa na wanamitindo wengi nchini wakiwemo Martin Kadinda, Jamila Vera Swai, Mkwandule Son, Kiulah, Lucky Creations, Enji Maasa na African Shiners.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Maonyesho ya Swahili Fashion, Mustafa Hassanali, alisema onyesho la mwaka huu litakuwa la aina yake ambalo litafana zaidi ya yaliyopita.
Alisema kwa mara ya kwanza onyesho hilo litaonyeshwa moja kwa moja katika televisheni ya Azam TV kwa ajili kuwapa fursa watanzania wote kushuhudia.
Hassanali alisema wabunifu mbalimbali wa mitindo kutoka katika nchi za Malawi, Nigeria, Afrika Kusini, Uganda na Kenya watashiriki.
Alisema onyesho la mwaka huu litawapa fursa wabunifu chipukizi kuonyesho uwezo wao katika jukwaa kuu.
Naye Mkurgenzi wa vipindi wa Azam TV, Charles Hillary alisema wameamua kuonyesha onyesho hilo moja kw moja kwa ajili ya kuwapa fursa watazamaji wake nchi nzima kushuhudia.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa ukuzaji sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Shaluwa, alisema serikali imembariki Hassanali kufanya onyesho hilo kwa ajili ya kukuza sekta ya sanaa ya ubunifu.
Alisema onyesho hilo litasaidia kukuza lugha ya kiswahili na utalii wa nchi kutokana na wabunifu kutoka nchi mbalimbali watashiriki.

KUHUSU SWAHILI FASHION WEEK
Swahili fashion week ni onyesho kubwa la mitindo na mavazi afrika mashariki na kati linaliofanyika kila mwaka, ni jukwakaa kubwa linalowapatia nafasi wabunifu wa mavazi na vito kutoka nchi za afrika masharika na zinginezo kuonyesha vipaji vyao, kutengeneza soko la ubunifu na kupata na kukuza mtandao wa wateja katika tasnia ya mitindo.
onyesho hili lina nia ya kusisitiza jamii kuwa mitindo ni pato linalozalisha tasnia ya ubunifu, wakati huo huo ikikuza dhana ya “bidhaa za afrika “. Swahili fashion week ni jukwaa la mitindo lilianzishwa mwaka 2008 na Mustafa Hassanali mbunifu kubwa na mkongwo afrika kutoka Tanzania.
Swahili Fashion Week ni jukwaa la mitindo lilianzishwa mwaka 2008 na mbunifu mkongwe na mashuguhuli kutoka Tanzania, Mustafa Hassanali
Onyesho la mwaka huu litakuwa onyesho la 10 toka lianze kufanyika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.