Habari za Punde

TASWA FC YAICHABANGA POLISI MABAO 5-0, TASWA QUEENS YACHEZEA KICHAPO

 DCP Mary Nzuki wa Jeshi la Polisi, akimkabidhi Ngao ya ushindi Nahodha wa Taswa Fc, Willbert Moland, baada ya Taswa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Polisi katika mchezo wa kirafiki wa Maadhimisho ya 10 ya Mtandao wa Polisi yaliyoanza leo mchana katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, yakitarajia kumalizika Nov 9 mwaka huu. Mabao wa Taswa yalifungwa na Zahro Milanzi mabao 4 na Ally bao 1. Na katika mchezo wa mpira wa pete kati ya Taswa Queens na Polisi Kombaini Polisi wameibuka na ushindi wa mabao 17 -13. Picha na  MAFOTO MEDIA GROUP
 Beki wa Taswa Fc, Muhidin Sufiani 'Mafoto' (kushoto) akijipinda kupiga mpira huku akizongwa na Hemed Yusuph wa timu ya Polisi wakati wa mchezo huo wa kirafiki wa Maadhimisho ya 10 ya Mtandao wa Polisi kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa wiki, Taswa Fc ilishinda mabao 5-0. 
 Mshambuliaji wa Taswa Fc, Said Seif (kushoto) akiruka kumkwepa beki wa Polisi Fc, Andew Thomas, wakati wa mchezo wa kirafiki katika Maadhimisho ya 10 ya Mtandao wa Polisi yaliyoanza leo mchana katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, yakitarajia kumalizika Nov 9 mwaka huu. Katika mchezo huo Taswa Fc ilishinda mabao 5-0.
 Hemed Yusuph wa Polisi (kulia) akijaribu kumpita Willbert Moland, wakati wa mchezo huo.
 Majuto Omary (kulia) akijaribu kumpia beki wa Polisi.
 Beki wa timu ya Soka ya wanawake ya Magereza, Victoria Lazaro (kulia) akiwania mpira na Farijika Miraji wa timu ya Soka ya wanawake ya Polisi, wakati wa mchezo wa maadhimisho ya 10 ya Mtandao wa Polisi yaliyoanza leo mchana Nov 4 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
 Chaliiiii
Hemed Kivuyo (kulia) naye alikuwepoooooo, Mkeyenge naye alikuwepoooooo...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.