Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (wa pili kushoto)hii leo amewasilisha taarifa
ya Utekelezaji wa Kamati ya Pamoja ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ya kushughulikia masuala ya Muungano kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria. Kutoka kulia ni Naibu
Katibu Mkuu Bi. Butamo Kasuka Phillip na Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Malongo.
Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Muungano Bw. Baraka Baraka.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi
ya Makamu wa Rais wakifuatilia majadiliano katika kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Katiba na Sheria Bi. Najma Murtaza Giga (kulia) akiongoza kikao cha Kamati
yake wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Kamati ya pamoja ya
masuala ya Muungano. Kushoto ni Bw. Dunford Mpelumbe Katibu wa Kamati.
No comments:
Post a Comment