Habari za Punde

YANGA YABANWA MBAVU NA SINGIDA UTD, YAKAA KILELENI KWA MUDA

Timu ya Yanga leo imebawa mbavu na Singida Utd baada kutoka suluhu bila kufungana katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Namfua jioni ya leo. Pamoja na kuwa mchezo huo ulikuwa na spidi na msisimko wa hali ya juu lakini hadi zinamalizika dakika 90 timu hizo zilishindwa kufungana.
Baada ya mchezo wa leo Yanga imekaa kileleni ikifikisha jumla ya Pointi 17, sawa na Mtibwa Sugar yenye pointi 17 pia huku simba wakirudi nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 16, nafasi ya Nne wakibaki Azam Fc ambao wanashuka dimbani usiku huu kukipiga na Ruvu Shooting.

MATOKEOYA MECHINI NYINGINE:
Kagera Sugar 1 - Tanzania Prisons 1
Njombe Mji 0 - Mbao Fc 0
Azam Fc 1- Ruvu Shooting 0
Singida Utd 0 - Yanga SC 0

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.