Habari za Punde

YANGA YAGOMEA PINGU ZA TANZANIA PRISONS YACHOMOA 1-1

TIMU ya Yanga jioni ya leo imeshindwa kutumia vyema uwanja wa Chamazi jijini Dar esSalaam, kama wenyeji wa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1.
Katika mchezo huo Tanzania Prisons walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 7 kupitia kwa mshambuaji wao, Eliuta Mpepo na Yanga wakafanikiwa kusawazisha katika dakika ya 42 kupitia mpira uliopigwa na kiungo wake Raphael Daud na beki wa Prisons akajifunga. 
Katika mchezo mwingine Singida Utd wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.
Mbao Fc 1 -Mwadui Fc 0
Ruvu Shooting 2 - Majimaji 1
Kagera Sugar 0 - Stand Utd 0
Yanga Sc 1- Tz Prisons 1

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.