Habari za Punde

BAADA YA KUTOKA JELA BABU SEYA AWA LULU, AFICHWA HOTELINI

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mitaa ya jiji la Dar es Salaam, juzi ililipuka kwa shangwe za kila aina mara tu baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza msamaha kwa wafungwa, wakiwemo wanamuziki baba na mwana, Babu Seya na Papii Kocha.
Hali hiyo iliibuka katika mitaa mbalimbali na hata katika maofisi kadhaa ambapo badhi ya wafanyakazi walishindwa kuendelea na kazi kwa mshtuko wa kile ambacho hakikutarajiwa na wengi kutokana na Mwanamuziki huyo kuwa alifungwa kifungo cha maisha.
Baada tu ya msamaha huo wanananchi wengi na baadhi ya wasanii walifurika nje ya jengo la Magereza Ukonga ili kumlaki Babu Seya na mwanae Papii Kocha, lakini walikatishwa tamaa na wengine kutawanyika baada ya kutangaziwa kuwa isingekuwa rahisi kuachiwa kwa siku hiyo (juzi) kutokana na taratibu za Magereza.
Mnamo majira ya saa 12 jioni zilianza kusambaa picha katika mitandao ya kijamii akionekana Babu Seya na Papii Kocha wakipunga mkono nje ya gereza hilo kuashiria furaa waliyokuwa nayo kwa kuanza kuwa huru wakielekea nyumbani kuanza maisha mapya baada ya kupata msamaa huo.
Kama ilivyo ada ya watanzani walianza kufurika palipokuwa nyumbani kwake mitaa ya Sinza wakijiandaa kumpokea bila kujua kuwa hawatafikia katika nyumba hiyo jambo ambalo liliwaacha na butwaa wananchi waliokuwa wamefurika katika nyumba hiyo juzi usiku.
Siku ya pili baada ya msamaha huo Gazeti hili lilifanya jitihada za kumpata Babu Seya bila mafanikio kutokana na kwamba ilielezwa kuwa iliyokuwa nyumba ya mwanamuziki huyo iliyo mitaa ya Sinza ilishauzwa kwa mmiliki wa Kampuni ya Global Publishers, huku ikielezwa kuwa baada ya kutoka Ukonga wanamuziki hao walielekea Katika Kanisa lililopo mitaa ya Tabata kupata ibada.
Aidha ilielezwa kuwa baada ya wanamuziki hao kutoka Kanisani hawakufikia tena katika nyumba hiyo iliyoelezwa kuuzwa wala kwa mtoto wao Nguza Mbangu aliyeachiwa kabla yao ambaye anaishi mitaa ya Tabata na badala yake walipelekwa katika moja ya Hoteli iliyopo mitaa ya Tangbovu ambako wapo hadi hii leo.
Akizungumza na Mtandao huu, mmoja kati ya wasanii walio katika Kamati ya kuratibu shughuli za mwanamuziki huyo baada ya kutoka jela, ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini, alisema kuwa Babu Seya anatarajia kuanza kuzungumza leo jumatatu baada ya kamati hiyo kukutana jana na kupanga ratiba yake ya maisha mapya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.