Habari za Punde

BABU SEYA APATA MSIBA MZITO SASA KUTIMKIA CONGO???

 Na Muhidin Sufiani, Dar
IKIWA ni siku tatu tu baada ya kutoka jela familia ya msanii nyota wa muziki wa dansi  nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ imepata msiba mzito  baada ya msanii huyo kufiwa na mdogo wake.
Imeelezwa ,  chanzo cha kifo ni mshituko uliotokana na furaha kubwa  aliyoipata marehemu ambaye ni mdogo wake baada ya kupata taarifa za kutolewa gerezani kwa Babu Seya  na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.
Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu umezipata Dar es Salaam, leomchana ,  kutoka kwa mmoja wa ndugu wa karibu wa familia hiyo, aliyeomba jina lake kutokutajwa kwa kuwa yeye si msemaji wa familia zilisema, msiba huo umetokea juzi, jana Congo, aliko zaliwa Babu Seya.
Chanzo hicho cha habari kilisema kifo hicho kimetibua kabisa furaha ya kuachiwa huru kwa Babu Seya pamoja na familia nzima.
“Alifariki muda mfupi baada ya kupata taarifa za kuachiwa kwa kaka yake (Babu Seya) na mwanaye (Papii Kocha). Furaha ilizidi,” kilisema chanzo chetu.
Mtoa habari huyo alisema, msiba huo ni mzito kwani marehemu ni ndugu wa damu na Babu Seya ingawa hakutaka kumtaja kwa jina.
“Familia iko katika majonzi mazito kwa sasa. Hili ni pigo zito na tunaangalia uwezekano wa kwenda Congo kwa sababu marehemu alikuwa ni sehemu ya familia,” alieleza.
Aliongeza; “Mimi siwezi kuongea mengi ila mkimtafuta King Kii (Kikumbi Mwanzampango) ndiye anaweza kuwapa maelezo zaidi,”.
Mtandao huu ulimtafuta mwanamuziki King kii, ambaye alieleza kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo la msiba mpaka apate ridhaa ya familia ya Babu Seya.
“Sawa pamoja na kwamba mimi ni mtu wa karibu na familia na ninahusika na suala hili lakini ngoja kwanza nipate ridhaa ya familia. Kuna msemaji wa familia Nguza Mbangu,”alieleza King Kikii aliyewahi kutamba na wimbo wa Kitambaa cheupe.
 “Nyie si mnataka kuandika katika gazeti kuhusu msiba? Lazima niombe ridhaa ya familia. Nikiongea na familia kisha nitarejea kwenu kuwapa majibu,”alifafanua.
Baada ya muda Mtandao huu ulimtafuta tena King Kii, na kuweka wazi kuhusu msiba huo akithibitisha kwa kusema ‘’ni kweli msiba wa mdogo wake Babu Seya umetokea huko Congo, katika Mji mkuu wa Lubumbashi Mkoa wa Katanga, jana na sababu tulizozipata inaelezwa ni mshtuko wa furaha baada ya kusikia Babu Seya ameachiwa huru’’. Alisema King Kii
Wakati hayo yakiendelea, leomchana, kulikuwa na taarifa za Babu Seya na Papii Kocha, kutembelea katika ofisi  za kampuni moja ya  habari iliyopo Sinza.
Hata hivyo Mtandao huu ulielezwa kuwa mkakati huo unafanyika kwa siri  mno baina ya familia ya Babu Seya na wahusika wa ofisi hiyo na kwamba gari lenye vioo vya giza ndiyo lingewapeleka mahala hapo ili kukwepa macho yawatu.
Chanzo chetu cha habari kilieleza, familia hiyo ilipanga kutumia chombo hicho cha habari kuzungumza kwa mara ya kwanza tokea  Babu Seya na Papii Kocha walipotoka gerezani Desemba 9 mwaka huu kwa msamaha wa Rais Dk. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
“Hata wafanyakazi wa kampuni hiyo ya habari wanawasubiri kina Babu Seya. Lakini kutokana na msiba huenda ratiba hiyo ikaenda ndivyo sivyo  kwa sababu kuna mambo mawili.
Lakwanza ni familia kuwa katika mkakati wa kusafiri kwenda Congo  kwenye msiba au kutokwenda  huko ili waendelee na ratiba za hapa,” kilieleza chanzo chetu cha habari.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.