Habari za Punde

BALOZI WA CHINA NCHINI AKUTANA NA MAKAMU MWENYEKITI CCM BARA

 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke, aliyefika Ofisi ndogo za CCM Makao Makuu Lumumba jijini Dar es Salaam  kwa mazungumzo. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Balozi  wa China nchini Tanzania, Wang Ke, akifafanua jambo kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, wakati wa mazungumzo yao Ofisi ndogo za CCM Makao Makuu Lumumba jijini Dar es Salaam
  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, akifurahi wakati akipokea zawadi ya picha ya Daraja la China lenye historia na makumbusho ya nchi hiyo, kutoka kwa Balozi Wang ke, baada ya mazungumzo yao.
 Mazungumzo yakiendelea baina ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na Balozi, Wang Ke. Kushoto ni wasaidizi wa Balozi.
Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke, akipokelewa na Katibu Msaidizi Idara ya Siasa  na Mahusiano ya Kimataifa CCM, Imanuela Kaganda, alipowasili ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam jana. Kushoto pia ni Katibu Msaidizi Idara ya Siasa  na Mahusiano ya Kimataifa CCM, Deborah C. Kiyuga.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, akipiga picha ya kumbukumbu na balozi wa China, Wang Ke, baada ya mazungumzo yao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.