Habari za Punde

BREAKING NEEEEEWZZZZ!!!! BABU SEYA, PAPII KOCHA WAACHIWA HURU

MWANAMUZIKI maarufu nchini Babu Seya na mwanawe Papy Kocha, wameachiwa huru leo kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais ametangaza msamaha huo leo katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tannzania, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Babu Seya na mwanawe Papii Kocha walitiwa hatiani miaka 13 iliyopita.
Katika msamaha huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli, ametoa msamaha kwa wafungwa 8157 ambapo wafungwa 1828 wataachiwa huru leo na 6329 watapunguziwa muda wao wa kifungo, Pia ametoa msamaha kwa wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa na kuziagiza idara husika kuwatoa leo au kesho.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa Tanzania tuna wafungwa 39,000 mpaka jana, kati ya hao 37,000 ni wanaume na 2,000 ni wanawake huku Wanaosubiri kunyongwa wakiwa ni 522, wanaume 503, wanawake 19 tu. Nguza Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha), ambao walihukumiwa kifungo cha maisha miaka 13 iliyopita, hivyo kuanzia leo familia hiyo iko huru.
HABARI KAMILI ITAFUATA KAA NASI.....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.