Habari za Punde

GEORGE WEAH ATANGAZWA URAIS LIBERIA

MWANASOKA wa zamani wa Dunia, timu ya Taifa ya Liberia, Klabu ya Man City, Monaco ya Ufaransa George Weah, leo ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa nchi yake ya  Liberia.
George Weah mwenye umri wa miaka 51, ametangazwa mshindi baada ya na kuwa rais wa Liberia baada ya kushinda majimbo 12 kati ya 15 ya nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika, akimbwaga m
pinzani wake, Joseph Boakai (73) na Makamu wa Rais wa sasa, akipata majimbo mawili tu.
Mwafrika huyo pekee kushinda Ballon d’Or, Weah aliyewahu kuwika na Klabu za AC Milan, Paris Saint-Germain, Marseille za Ufaransa, AC Milan, Chelsea na ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwashukuru mashabiki akisema amepanga kuleta mapinduzi katika nchi hiyo.
Kwa ushindi huo, mshambuliaji huyo aliyegeukia siasa anakuwa rais wa 25 wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.