Habari za Punde

IGP SIRRO AKAGUA NA KUSHIRIKI MAZOEZI YA UKAKAMAVU NA ASKARI WA MKOA WA TABORA.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu toka kulia alishiriki mazoezi ya utayari na kuwatia hamasa Askari wa Mkoa wa Tabora, katika ziara yake ya siku moja mkoani humo, hatua hiyo ni kutokana na kuwataka askari wa Jeshi la Polisi kuwa na utayari wakati wote . 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiwa amembeba Joshua mtoto wa muumini wa kanisa la Siroham mkoani Tabora kabla ya uzinduzi wa zahanati ya Polisi iliyojengwa kwa hisani ya kanisa hilo. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu kutoka kushoto akiangalia mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi akiwa katika mazoezi ya utayari kupita juu ya kamba mkoani Tabora . Picha na Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.