Habari za Punde

KAMERA YA MAFOTO BLOG MITAANI LEO, ABIRIA WA KAGERA WAKWAMA UBUNGO

Baadhi ya mabasi ya abiria yakiwa yamebaki machache katika Kituo cha Mabasi Ubugo kuelekea kipindi cha sikukuu kutokana na baadhi ya Kampuni za Mabasi kufungiwa na SUMATRA na TRAFFIC kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani. Kutokana na hatua hiyo baadhi ya mabasi yamepandisha nauli za kwenda mikoani.
***************************
Leo asubuhi baadhi ya abiria wanaosafiri kwenda mkoani Kagera wamekwama katika kituo hicho na kuomba msaada baada ya basi lao walilokuwa wasafiri nalo la  Kampuni ya  RS leo Saa 12:00 asubuhi, lilikwama Ubungo. 
''Tulipofika alfajiri wakatuambia tusubiri  gari linakuja, mpaka  saa 02:00 asubuhi hatukuona hata dalili za gari,  Baadaye wakatuambia  gari limeharibika hivyo tutaondoka na gari la Kampuni ya Osaka,
Mpaka majira ya saa sita bado abiria hao walikuwapo kituoni hapo bila kupata gari hilo, ambapo pia imeelezwa kuwa SUMATRA walifika eneola tukio na kuondoka bila kuwasaidia abiria hao waliokwama.

Tunaomba msaada wa Waandishi wa Habari tafadhali maana tupo hapa tunanyeshewa mvua tangu asubuhi'' alisikika mmoja wa abiria hao

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.