Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KITAIFA JIJINI DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TAYOA Bw. Peter Masika wakati alipotembelea banda la TAYOA wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo kitaifa yalifanyika jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Da es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama ramani inayoonyesha maeneo yalioathirika na ugonjwa wa ukimwi ambayo yameainishwa kwenye  taarifa ya Utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi Tanzania (THIS) wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo Kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ramani inayoonyesha maeneo yalioathirika na ugonjwa wa ukimwi ambayo yameainishwa kwenye  taarifa ya Utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi Tanzania (THIS) wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo Kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa UNAIDS Dkt. Leo Zekeng mara baada ya uzinduzi wa taarifa ya Utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi Tanzania (THIS) wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo Kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.