Habari za Punde

MASHINDANO YA QUR-AN NA QASWAIDA KWA MABINGWA WA TANZANIA NA IRANI YAFANYIA DAR

 Mgeni rasmi Prof. Juma Kapuya, akizungumza wakati wa mashindano Qur-an na Qaswaida kwa mabingwa wa Tanzania na Iran, yaliyofanyika jana usiku katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mussa Farhang (kushoto) akisalimiana na mgeni rasmi, Prof. Juma Kapuya, (katikati) wakati wa mashindano ya Qaswaida na kuraan yaliyowakutanisha mabingwa wa Tanzania na Iran yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kulia ni Sheikh kutoka Iran, Ibrahim Surkh.
 Sheik Hassan Shaha wa Madrasat Maamul ya Temeke akisoma Qur aan wakati wa mashindano hayo na kukonga mashabiki waliokuwapo ukumbini hapo.
 Mmoja kati ya washiriki kutoka Iran akirekebisha mitambo mwenyewe baada ya kuona watanzania wakishangiliwa wakati wa mashindano hayo ili kuongeza eko.
 wageni kutoka Iran
 Baadhi ya watanzania waliofika kushuhudia mashindano hayo
  Baadhi ya watanzania waliofika kushuhudia mashindano hayo
  Baadhi ya watanzania waliofika kushuhudia mashindano hayo
 Wageni waalikwa pamoja na mgeni rasmi Prof Juma Kapuya
 Mshiriki wa Tanzania, ambaye ni aliwahi kuwa mshindi wa sita katika mashindano ya kusoma Qur aan ya Dunia, yaliyofanyika nchini Iran mwaka 2016 Rajai Ayoub, akisoma Qur-aan wakati wa mashindano hayo.
 Rajai akipongezwa na Sheikh Hemed Jalala (kushoto) na Sheikh Mohamed Abdi baada ya kumaliza kusoma.

 Washieiki kutoka Iran kikundi cha Misbahul Huda wakifanya ya kwao mbele ya mashabiki katika ukumbi wa Kituoc ha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Mshiriki wa Tanzania, kwa upande wa Qaswaida, Salim Seif Hurairah akiimba qaswaida yake mpya kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo.
 Mshiriki kutoka Iran, Adnan Muumin, akisoma Qur aan wakati wa mashindano hayo.
 Washiriki wa Tanzania wakimba qaswaida ya kutumia ala za muziki
Mgeni rasi Prof Juma Kapuya akiagana na mc Saleh Omar

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.