Habari za Punde

MICHEZO NI AFYA KWA TAIFA: WAZIRI MWAKYEMBE

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia.) akiwa katika picha ya pamoja na timu iliyoshinda fainali za mashindano ya mabenki yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru aliyeshika kombe ni Kapteni wa Timu hiyo Bw.David Kikambako na (wa kwanza kulia ) ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhi zawadi ya mchezaji bora wa mashindano Bw.Jesse Nyambo kutoka Benki ya  Exim (katikati) ni muundajia wa mashindano hayo Bi.Nasikiwa Beria.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhi zawadi ya cheti cha Kapteni bora  wa mashindano ya Mabenki Bw.David Kikambako kutoka benki ya DTB wa Exim Bank (katikati) ni muundajia wa mashindano hayo Bi.Nasikiwa Beria.
Mshambuliaji wa timu ya Benki ya Exim Abdallah Masoud (Katikati) akipambana katika mchuano wa fainali za mashindano ya Mabenki
*******************************************
************************************
Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ameto wito kwa sekta mbalimbali nchini kutoa fursa za wafanyakazi wake kushiriki katika michezo wawapo kazini kwani michezo ni afya.
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa wito huo alipokuwa akifunga fainali za mashindano ya michezo ya  mabenki yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Uhuru.
“Natoa pongezi kwa taasisi zote benki zilizoshiriki katika mashindano haya kwa michezo ni afya na inaongeza utendaji mzuri kazini pamoja na kuongeza umoja miongoni mwa wafanyakazi,”Mhe.Dkt. Mwakyembe.
Naye Muandaaji wa mashindano hayo Bi Nasikiwa Beria alisema kuwa anashukuru serikali kwa kuwaunga mkono na katika mashindano hayo kwani imewapa hamasa zaidi na kwa mwakani watajitahidi mashindano haya yafanyike pia na mikoani tofauti na mwaka huu yalivyofanyika hapa jijini Dar es Salaam.
“Mashindano haya kwa mwaka huu yalihusisha benki kumi na tano  na kulikuwa na michezo sitini na tulianza michuano kuanzia mwezi wa nane na fainali ndiyo zimefanyika mwezi huu Desemba na kwa mwakani tunampango wa kuongeza michezo iwe ya aina mbalimbali ikiwemo Volleyball na Netiboli,”Bi.Beria.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Exim Benki ambaye jina lake halikuweza kujulikana kwa haraka alitoa pongezi na zawadi ya shilling laki moja kwa kila mchezaji wa timu ya ofisi yake kwa kuibuka washindi wa pili katika mashindano hayo .
Pamoja na hayo na Kapteni wa Timu  ya DTB Benki Bw.David Kikambako alishukuru viongozi wa benki zilizoshiriki kwenye mashindano hayo na kutoa wito kwa benki nyingine kujitokeza kujiunga katika mashindano hayo kwa mwakani .

Katika mashindano hayo Benki ya DTB iliibuka kidedea kwa penati tatu dhidi ya Timu ya Exim Benki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.