Habari za Punde

MWANAMUZIKI NCHINI MISRI ATUPWA JELA MIAKA MIWILI KWA KULA NDIZI VIEONI

Shyma wrote that she had not anticipated the backlash against her video .
******************************
Mahakama nchini Misri inaripotiwa kumtupa jela mwanamuziki mmoja wa kike miaka miwili baada ya kuonekana kwenye video yake ya muziki akiwa na vazi la ndani haku akila ndizi.
Shyma Ahmed, 25, ambaye kimuziki anafahamika kama Shyma, alikamatwa mwezi uliopita baada ya video hiyo kuzua ghadhabu kwenye taifa hilo.
Siku ya Jumanne alipatikana na hatia ya kuunga mkono mapenzi na kwa kuchapisha video inayokiuka maadili.
Mwongozaji wa video hiyo pia alihukumiwa kifungo cha miaka miwili licha ya yeye kutokuwepo mahakamani hapo.
Shyma aliomba msamaha kabla ya kukamatwa kwake lakini agizo la kuendelea kumsaka na kutiwa guvuni liliendelea hadi alipopatikana.
"Sikufikiria haya yote yatafanyika na kwamba ningeshambuliwa kwa kiasi hiki kutoka kwa kila mtu." alisema shyma
Mwaka uliopita mahakama nchini Misri ilawahukumu wacheza dansi watatu wanawake miezi sita gerezani baada ya kuwatuhumu kwa kuchochea ngono kwenye video ya muziki.
Mwimbaji mwingine anakabaliwa na kesi kwa kueneza uvumi kuwa maji ya mto Nile yanaweza kumfanya awe mgonjwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.