Habari za Punde

NORWAY YATOA ZAIDI YA BILIONI 13 KUSAIDIA UKANDA WA AFRIKA MASHAIKI

Balozi wa Norway nchini, Hanne Marie Kaarstad, akisainiana hati za makubaliano na Mwenyekiti wa Bodi ya Trademark East Africa, Ali Mufuruki, zaidi ya sh. Bilioni 13 ikiwa ni msaada kwa ajili ya kuimarisha biashara Ukanda wa Afrika Mashariki. Hafla hiyo ilifanyika Ofisi za Ubalozi huo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Trademark East Afrika, John Ulanga (kulia) ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano, Trygve Bendiksby. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
UBALOZI wa Norway nchini umefadhiri kiasi cha zaidi ya Sh Bilion 13 kwa kampuni ya Trademark East Africa (Tanzania) ikiwa ni jitihada za kuwaunga mkono katika kuimarisha biashara ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya msaada huo kwenye ofisi za Ubalozi wa Norway  nchini, Balozi Mkazi wa Norway Hanne Marie amesema Ubalozi umeguswa na kazi nzuri inayofanywa na Trade Mark East Africa.
"Ubalozi umevutiwa na kazi nzuri iliyofanywa na  Trade Mark East Africa katika utekelezaji wa kizuizi cha pamoja cha mpakani na kuunganishwa kwa mfumo mzuri katika mipaka ya Mtukula, Kabanga na Holili ambapo uboreshaji wa mipaka hiyo umekuwa na ufanisi mkubwa.
Balozi huyo ameongeza kuwa alikuwa akifuatilia kwa umakini mkubwa miradi iliyokuwa ikitekelezwa na Trademark nakubaini kuwa kuna maboresho makubwa katika maeneo wakiyafanyia kazi hususani bandari ya Dar es Salaam ambapo kulikuwa na utitiri mwingi wa ushuru.
Balozi Marie ameongeza kuwa wameamua kuwaunga mkono katika jitihada za kutengeneza mazingira mazuri ya biashara mipakani,nakuwaunga mkono katika kampeni iliyozunduliwa hivi karibun itwayo mwanamke na biashara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Ali Mfuruki amesema kuwa Trade Mark East Afrika hufanya shughuli zake kwa ufanisi wa hali ya juu lengo likiwa nikupunguza vikwazo vya kibiashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.
" Kazi yetu nikutekeleza kwa ufanisi kile tulichopanga kutekeleza lakini pia kuona matokeo chanya,tunashukuru kuona Ubalozi umeona kazi nzuri tuliyofanya nakuamua kutuunga mkono.Amesema.
Kuanzia kuanzishwa kwake 2011 TradeMark imepunguza vizuizi vingi vilivyo kuwa vikikwamisha maendeleo ya biashara matharani Uboreshwaji wa Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam,Mamlaka ya Mapato Tanzania,Mamlaka ya Chakula na Dawa na Shirika la Viwango Tanzania.
Makabidhiano
Mkurugenzi Mkazi wa Trademark East Afrika, John Ulanga, akizungumza
Mkurugenzi Mkazi wa Trademark East Afrika, John Ulanga, akielekezana jambo na Johanne Walthinsen
Ali Mufuruki akitoa shukrani zake kwa Ubalozi wa Norway baada ya makabidhiano hayo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.