Habari za Punde

QUEENELIZABETH MAKUNE AIPAISHA TANZANIA ATWAA TAJI LA MISS WOLRD UNIVERSITY AFRICA'

Mrembo wa Tanzania, Miss World University Africa, Queenelizabeth Makune, akipozi na Taji lake baada ya kutangazwa mshindi katika shindano la Dunia lililofanyika nchini Korea usiku wa kuamkia jana. Mrembo huyo anatarajia kuwasili nchini keshokutwa jumamosi.
 BAADA ya miaka 12  tangu aiwakilishe vyema Tanzania kwenye mashindanoya urembo kimataifa, Mrembo Nancy Sumari, katika shindano la urembo la Dunia na kuibuka na Taji la Miss World Afrika 2005 hatimaye Taji hilo limetua tena Afrika kupitia kwa Mrembo QueenElizabeth Makune wa Tanzania ambaye usiku wa kuamkia leo ametangazwa mshindi wa 'Miss World University Africa' katika shindano la 28 la World Miss University lililofanyika nchini Korea.
Shindano hilo limeshirikisha warembo mbalimbali, kutoka katika mataifa 102, huku kati yao yakiwamo Mataifa 53 ya Afrika ambayo yameongozwa na mrembo huyo, Queenelizabeth aliyeshika namba moja kati ya 53.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.