Habari za Punde

RAIS KARIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA LIMONGA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mtangazaji wa Kituo cha Radio Uhuru, Limonga Justin Limonga kilichotokea leo Desemba 31, 2017 kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar Es Salaam.
Kutokana na msiba huo, Rais Karia ametuma salamu za rambirambi kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho cha Radio, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) pamoja na wanafamilia wote wa mpira wa miguu na wasikilizaji wote wa Radio Uhuru.
Rais Karia amesema anatambua mchango wa Limonga na Radio Uhuru katika kupasha habari za michezo kupitia Radio hiyo.
Hivyo, ameguswa na kuona kuwa tasnia ya michezo na habari imepoteza hazina nyingine, lakini ametoa wito kwa wadau, familia ya Limonga, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwao.
Karia amesema kwamba hatuna budi kuwa na imani kama maandiko yanavyosema kwamba Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Mkutano wa mwisho kwa Limonga kuhudhuria ulikuwa Januari 27,2017 wakati Rais wa TFF Wallace Karia alipokutana na Wahariri wa Habari za Michezo kwenye Hoteli ya SeaScape.
……………………………………………………………………..……………..……
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.