Habari za Punde

RAIS WA ZANZIBAR AWAZAWADIA WACHEZAJI WA ZANZIBAR HEROES

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakiwa wamesimama wakati ukipingwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya chakula maalum na kuwazawadia wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes.

Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakiwa wamesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa Hafla hiyo ya Chakula cha usiku na kukabidhiwa zawadi zilizoahidiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Ikulu juzi wakati wa chakula cha mchana.
Kikundi  cha Taifa cha Taarab Zanzibar kikitowa burudani wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
Baadhi ya wachezajiI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakifurahia ushindi wao wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili yao.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wakati wa hafla ya chakula maalum alichowaandalia na kuwakabidhi zawadi.Picha na Ikulu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.