Habari za Punde

TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WANAOTUMIA MFUMO WA MALIPO WA E-PAYMENT

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa taarifa ya kuomba radhi wateja wanaotumia mfumo wa "e - payment" ili kuunganishiwa umeme "service line" kwa kushindwa kupata huduma hiyo kutokana na hitilafu iliyotokea katika mfumo huo. 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 30, 2017 na Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO, Bi. Leila Muhaji, wataalamu wa Tehama (ict) wa Shirika hilo wanaendelea na jitihada za kurekebisha hitilafu hiyo ili kuurejesha mfumo katika hali yake ya kawaida. “Tutaendelea kutoa taarifa zaidi na kwa mawasiliano toa taarifa kupitia, kituo cha miito ya simu makao makuu 0222194400 na 0768 985100 tovuti: www.tanesco.co.tz mitandao ya kijamii www.facebook/twitter.com/tanescoyetu.” Amesema Bi. Leila na kuongeza uongozi wa Shirika hilo unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.