Habari za Punde

WAZIRI JENISTA AKAGUA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA UHURU MJINI DODOMA

 Askari Makomandoo wa Jeshi la ulinzi (JWTZ) wakionyesha umahiri wao wa kushuka kwa kamba kutoka kwenye Helkopta iliyo angani wakati wa maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikagua maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri  leo Mjini Dodoma.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri leo Mjini Dodoma.


Halaiki ya wanafunzi  wa shule za msingi na sekondari wakiunda umbo lililoonesha ramani ya Tanzania wakati wa  maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri  leo Mjini Dodoma.

 Gwaride la Mkoloni kutoka Jeshi la Polisi likionesha umahiri wake  ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri  leo Mjini Dodoma.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wanaoongoza misafara ya Viongozi wakionesha  umahiri wao katika kutekeleza majukumu yao ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo Mjini Dodoma. Picha na Beatrice Lyimo, MAELEZO, DODOMA

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.