Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA KAMPENI YA UZALENDO

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe akiwapongeza wajumbe wa kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo kwa ubunifu waliyoufanya katika siku ya uzinduzi uliyofanywa hivi karibuni na Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika kikao cha tathimini  ya uzinduzi wa Kampeni hiyo  kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi,Leah Kihimbi ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sanaa  kutoka Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi.Shani Kitogo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bi.Leah Kihimbi ambaye ni Mkurugenzi  Msaidizi Idara ya Sanaa  kutoka Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akieleza mafanikio ya uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) ikiwemo kupokea maombi kutoka taasisi mbalimbali kuomba wanakamati kwenda kutoa mafunzo kuhusu suala la uzalendo kwa watumishi wa ofisi zao,katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa Kampeni hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bi.Joyce Fissoo ambaye ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini akitoa mapendekezo katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu makala ya viongozi na wadau waliyozungumzia suala la uzalendo kwa taifa itakapo kamilika iweze kusambazwa nchini nzima katika shule za msingi na sekondari kwa ajili ya kuwapa fursa watoto hao kujifunza kuhusu uzalendo video.
Mjumbe wa Kamati ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo Bw.Mrisho Mpoto akitoa maoni ya mambo mbalimbali yanayoweza kufanikisha kampeni hiyo kuwa endelevu ikiwemo wajumbe kufanya tafiti kwa nchi zenye uzalendo kama China kwa lengo la kuhakikisha taifa linaelewa umuhimu wa uzalendo na manufaa yake katika kikao cha tathimini ya uzinduzi wa kampeni hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Anitha Jonas – WHUSM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.