Habari za Punde

YANGA YAPEWA KUANZA NA WASHELISHELI KLABU BINGWA AFRIKA, SIMBA YAPEWA WADJIBOUT

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga wamepangwa kuanza na timu ya St Lous ya Seychelles katika mchezo wa raundi ya kwanza katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Endapo Yanga kama itafanikiwa kufuzu katika mchezo huo wa raundi ya kwanza itakuwa na kibarua kingine cha kucheza na mshindi kati ya El Merreikh ya Sudani au Township Rollers ya Botswana.
Yanga imefanikiwa kucheza kombe la klabu bingwa barani Afrika baada ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/18.
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya soka ya Simba imepangwa kuanza na timu ya Gendermerie Tnale ya Djibout katika mchezo wa raundi ya awali ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Endapo kama wekundu hao wa msimbazi watafuzu katika mchezo huo wa raundi ya awali basi wakuwa na kibarua kingine cha kucheza na mshindi kati ya El Masry ya Misri au Green Button Aloes ya Zambia.
Simba imefanikiwa kupata nafasi ya kucheza kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuwa mabingwa wa kombe la Azam Sports Federation.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.