Habari za Punde

CAF YAMTEUA RAIS KARIA KUSIMAMIA CHAN

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Ndugu Wallace Karia ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Fainali za Africa kwa wachezaji wa ndani CHAN kati ya Morocco na Mauritania itakayochezwa Januari 13, 2018.
Mchezo huo ambao Rais Karia atausimamia akiwa Kamishna utachezwa kwenye Uwanja wa nyasi asilia wa Mohamed V huko Casablanca.
Waamuzi watakaochezesha mchezo huo ni Janny Sikazwe kutoka Zambia atakuwa muamuzi wa katikati akisaidiwa na muamuzi msaidizi namba moja kutoka Kenya Marwa Aden Range na muamuzi msaidizi namba mbili akitokea Msumbiji Arsenio Chandreque Maringula wakati muamuzi wa mezani Louis Hakizimana akitokea Rwanda.
Mchezo huo unaohusisha timu mwenyeji unatarajiwa kufuatiliwa na mashabiki wengi zaidi.
Rais Karia hivi karibuni pia aliteuliwa na CAF kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo ya CHAN itakayoanza Januari 13 mpaka Februari 4, 2018.
Mashindano hayo yanayofanyika kwa mara ya tano(5) bingwa mtetezi akiwa DR Congo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.