Habari za Punde

JUMA MAHADHI ALIVYOWAOMBA RADHI MASHABIKI WA YANGA JANA

KIUNGO wa Yanga, Juma Mahadhi ameandika ujumbe mzito wenye dhamira ya kuwaomba radhi mashabiki na viongozi wa Yanga kwa kushindwa kuwaonyesha kile walichokitarajia kutoka kwake. 
Mahadhi alisajiliwa akitokea Coastal Union ya Tanga ambapo alionyesha uwezo mkubwa kabla hajatisha tena katika mechi za awali alipojiunga Yanga lakini baada ya muda alipotea na hakufanikiwa tena kurejesha kiwango chake. 
Katika ujumbe huo aliouandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Mahadhi alionyesha kuwa hajaridhika na kiwango chake huku akiwa mtu wa kukaa benchi katika kikosi cha kocha George Lwandamina. Ikumbukwe Mahadhi amekuwa akilalamikiwa mara kwa mara na mashabiki wa Yanga kutokana na kushuka kiwango chake ambapo aliwahi kuisabaisha Yanga kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-5 dhidi ya Simba katika Ngao ya Jamii baada ya kukosa penalti ya mwisho. 
Mchezaji huyo aliandika ujumbe huo akionyesha hafurahii kiwango chake kuwa kibovu tangu kuanza kwa msimu uliopita.
 "Assalam alaykum ndugu zangu katika Imani, haja yangu kwenu ni kuomba radhi kwa mashabiki wangu wote na wapenzi wote wa mpira wa miguu duniani, nakiri kufanya makosa hapo nyuma na nimejifunza mengi kupitia nyinyi nawaomba sana radhi. "Ombi langu kwenu mashabiki, viongozi na benchi la ufundi ni kwamba kijana wenu nahitaji msamaha kama niliwakosea bado nahitaji nafasi naamin siwezi kurudia kosa," aliandika Mahadhi. 
Mahadhi amekuwa na kiwango kibo tangu msimu uliopita ambapo baadhi ya taarifa zilidai ameshuka kiwango kutokana na kulewa sifa na kuendekeza starehe baada ya kuonyesha kiwango katika mechi za hatu ya makundi ya Michuano ya Kombe la Shirikisho mwaka juzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.