Habari za Punde

KAMATI YA MAADILI YAMFUGIA MAISHA MJUMBE WA KAMATI YA UENDESHAJI TFF APIGWA

MSIMAMIZI wa kituo cha Mtwara, Dustan Mkundi ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF amefungiwa maisha kujihusisha na soka na kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo.
Mkundi na wenzake wanne walifikishwa mbele ya Kamati ya Maadili ya TFF  kwa kosa la kughushi na udanganyifu wa mapato ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katia ya Simba na Ndanda FC uliochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara Desemba 30, 2017.
Akizungumza na mtandano huu, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Wakili Hamidu Mbwezeleni, amesema kamati yake imemkuta na hatia Mkundi na kumfungia maisha kujihusisha na soka na Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mtwara Kizito Mbano akafungiwa miaka mitano.
Pia Mbwezeleni amesema Muhasibu msaidizi wa Simba Suleiman Kahumbu na Katibu msaidizi wa Klabu ya Ndanda FC ya Mtwara Selemani Kachele hawakuwa na hatia.
“Sekretarieti iliondoa jina la Kahumbu kwenye mashtaka badala yake aligeuka kuwa shahidi katika kesi hiyo lakini Mkundi tulimkuta na hatia kwa sababu hesabu za mapato zilizopelekwa bodi ya ligi na TFF zimetofautiana,”
“Bodi ya ligi alipekeleka mapato ya sh milioni 37 lakini TFF aliwasilisha sh milioni 34 na timu za Ndanda na Simba zilipata mgao kutoka kwenye sh. milioni 37 hivyo udandanyifu ulifanyika katika mgao uliohusu TFF, BMT na TRA,” aliongeza Mbwezeleni.
Mbwezeleni alisema Mkundi aliwapelekea fomu nyingine Kahumbu na Kachele wamsainie kwa madai fomu za awali zilipotea na wawili hao waliisadia kamati kupata undani wa mapato lakini Mbano hakuwa tayari kukutana na kamati japo aliitwa mara tatu.
Aidha kamati hiyo imeitaka TFF kuhakikisha wanalifikisha suala hilo kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
Kamati ya maadili iko chini ya Mwenyekiti Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti Wakili Steven Zangira, wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhresa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.