Habari za Punde

MAAMUZI YA KAMATI YA MASHINDANO

Kikao cha kamati ya Mashindano kilichokutana Desemba 29, 2017 kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujadili mchezo namba 31 na 32 uliohusisha timu za Abajalo FC dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya na ule kati ya Mvuvumwa na JKT Ruvu katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) iliyokuwa ifanyike Desemba 20, 2017 kwenye Uwanja wa Uhuru na Chamazi.
Kamati ilikaa na kupitia taarifa mbalimbali za michezo hiyo.
Kamati kupitia kanuni ya 24 kifungu cha (1) katika mchezo kati ya Abajalo FC na Tanzania Prisons imeipa ushindi timu ya Tanzania Prisons baada ya kubaini Abajalo kukiuka kanuni hiyo.
Kwenye mchezo mwingine kati ya Mvuvumwa na JKT Ruvu Kamati baada ya kupitia na kujiridhisha imeipa ushindi timu ya JKT Ruvu baada ya Mvuvumwa pia kukiuka kanuni ya 24 kifungu (1).
Kwa maamuzi hayo timu za Tanzania Prisons na JKT Ruvu zinafuzu kwenda kwenye hatua ya tatu(3) ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.