Habari za Punde

MADAKTARI BINGWA WAFANYA UPASUAJI WA MOYO KWA WAGONJWA TAASISI YA (JKCI)

 Madaktari  Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa ambaye mshipa mkubwa unaosambaza damu upande wa kushoto  wa moyo umeziba upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting).
 Picha no. 3 Madaktari  Bingwa wa Usingizi na wagonjwa mahututi  wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiangalia jinsi moyo wa mgonjwa unavyofanya kazi (mapigo ya moyo)  kwa kutumia mashine maalum wakati mgonjwa huyo akifanyiwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting). 
Madaktari  Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Benjamin Bierbach wa nchini Ujerumani wakimfanyia upasuaji wa kuziba matundu ya moyo mtoto mwenye  umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.