Habari za Punde

MECHI YA AZAM VS YANGA KUPIGWA CHAMAZI JUMAMOSI SAA 10 JIONI

Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018 kati ya Azam FC na Young Africans utachezwa saa 10 jioni Azam Complex Chamazi.  Mchezo huo namba 115 utachezwa Jumamosi Januari 27, 2018.
Viingilio kwenye mchezo huo ni shilingi elfu kumi(10,000) kwa Jukwaa Kuu na shilingi elfu saba (7,000) kwa majukwaa ya kawaida. 
Waamuzi wa mchezo huo wote ni kutoka Dar es Salaam ambapo muamuzi wa kati ni Israel Nkongo akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Josephat Bulali na mwamuzi msaidizi namba mbili Soud Lila, mwamuzi wa akiba Elly Sasii wakati Kamishna wa mchezo huo ni Omar Abdulkadir.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.