Habari za Punde

MSUVA AAHIDI MAKUBWA KWA WATANZANIA KUTIMKA MOROCCO KUKIPIGA ULAYA

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Difaa Hassani El Jadidi ya Morocco, Saimon Hepigoli Msuva amesema anatarajia kukipiga soka la kulipwa barani Ulaya kabla ya mwaka haijaisha.
Kauli ya Msuva imetoka muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, akitokea Morocco kwa ajili ya mapumziko nchini.
Msuva amekuja mapumzikoni kutokana na mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Morocco kumalizika na kupisha michuano ya Kombe la CAN.
Nyota huyo amepachika mabao matano katika Ligi Kuu ya Morocco katika michezo 14 aliyocheza ambapo anayeongoza kwa mabao amefunga mabao nane.
Akizungumza baada ya kutua jijini Dar es Salaam leoa subuhi, Msuva amesema kwa kipindi cha nusu msimu alichocheza nchini Morocco tayari ameshapata ofa kadhaa kutoka Ufaransa na Hispania ambazo hakupenda kuziweka wazi akisema mudaa bado.
Alisema sababu ya kupata ofa katika klabu za ligi kuu za Hispania na Ufaransa ni kutokana na kiwango chake kuwa kikubwa ikiwemo kuingia katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo iliyowahi kumuibua nyota Marouane Chamakh aliyewahi kukipiga Arsenal ya England akitokea Bordeaux ya Ufaransa.
Alisema anaamini juhudi zake zinaweza kumfikisha mbali katika soka la kulipwa kwa kuwa anatamani kufikia hadhi za Mbwana Samatta na Victor Wanyama. 
Nyota huyo aliyetwaa kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita akiwa Yanga, alisema ligi ya nchini Morocco inachangamoto kubwa kutokana na wachezaji wengi kuwa na ufundi wa kucheza soka tofauti na nchi za Afrika Mashariki.
“Mpira una changamoto kubwa lakini nimejiandaa kukabiliana nazo, najiamini jinsi ya kucheza na ndio maana leo hii nipo katika kikosi cha kwanza cha kocha baada ya . Naamini kwa uwezo wa Mungu kabla ya mwaka haujamalizika nitakwenda kucheza soka kati ya Hispania au Ufaransa,” alisema Msuva.
Msuva amewataka wachezaji wanaocheza soka la nchini kujituma na kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta mafanikio katika soka ikiwemo kucheza Ulala kwa ajili ya kukuza majina yao na nchi.

Nyota huyo atakuwa nchini kwa mapumziko ya wiki mbili kutokana na mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Morocco kumalizika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.