Habari za Punde

MTANANGE WA AZAMF FC VS JAMHURI JANA, AZAM IKISHINDA MABAO 4-0

 Kipa wa Timu ya Jamhuri, Ali Khamis akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na mshambuliaji wa  Azam, Benard Arthur,ambao ulimshinda na kutinga wavuni na kuandika bao la kwanza katika dakika ya 26 ya mchezo huo uliochezwa jana katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar. Katika mchezo huo Azam Fc imeshinda mabao 4-0  michuano ya Kombe la Mapinduzi, goli la PIli limefungwa na Salmin Hoza dakika ya 48 na bao la Tatu la limefungwa dakika ya 56 na Yahya Zayd na bao la nne likifungwa na Peter Paul katika dakika ya 79.
 Wachezaji wa Timu ya Azam wakishangilia bao la nne lililofungwa na Peter Paul katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
 Beki wa Jamhuri,  Abdallah Juma, akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Azam wakati wa mchezo huo.
 Mshambuliaji wa Timu ya Azam, Bruce Kangwa, akiruka kiunzi cha Beki wa Jamhuri, Abdullatif Omar, wakati wa mchezo huo Kombe la Mapinduzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan. 
 Beki wa Jamuhuri, Yussuf Makame, akiokoa mpira wa hatari langoni kwake

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.