Habari za Punde

TAARIFA YA KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inapenda kuutaarifu umma wa watanzania kuwa, kutakuwa na kikao cha kawaida cha Baraza la Vyama vya Siasa, kitakachofanyika   Januari 18, 2018 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi. Kikao hichokitafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkwawa, uliopo katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Barabara ya Shaabani Robert mkabara na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa , Jijini Dar –es salaam.
Pamoja na ajenda zingine zilizoandaliwa, wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa watapata fursa ya kujadili mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria mpya ya Vyama vya Siasa, kujadili mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni za usajili wa Vyama vya Siasa na pia watafanya uchaguzi wa viongozi wa kamati za Baraza la Vyama vya Siasa.
Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa hutokana na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa, ambapo kila chama cha siasa huwakilishwa na wajumbe wawili walioteuliwa na chama husika. Baraza la vyama vya Siasa ndicho chombo maalumu cha kisheria ambacho hutumiwa na vyama vya siasa kujadili masuala mtambuka ya kisiasa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.