Habari za Punde

TRL YATANGAZA MABADILIKO YA RATIBA ZA USAFIRI TRENI YA BARA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (Uendeshaji) Focus Sahani, akizungumza na waandishi wa habari.
*********************************************
 Na  Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imesema imeamua kuhamishia huduma ya usafiri wa treni kutokea mkoani Dodoma kuanzia kesho badala ya Dar es salaam kama ilivyozoeleka.
Uamuzi huo unakuja kipindi ambacho TRL imesitisha huduma za usafiri huo kutokea Dar es Salaam baada ya miundombinu ya reli kuharibika kati ya  stesheni za Kilosa na Gulwe   kutokana na mafuriko ya mvua zinazonyesha maeneo hayo na kuharibu miundombinu. 

Sehemu ya miundombinu ya reli iliyoharibika 
******************************
Akizungunza na waandishi wa habari kutoa ratiba za usafiri huo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi  Mkuu Msaidizi (uendeshaji) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuuu wa kampuni hiyo, Focus Sahani amesema wakati wanaendelea na matengenezo ya miundombinu iliyohariviwa na mafuriko eneo hilo wameona ni vema usafiri huo ukaendelea kwa kuanzia Mkoa wa Dodoma. 
Amesema uongozi baada ya kutathimini hali ya miundombinu ya maeneo mengine yaliyo salama imeamua kuhamishia huduma ya usafiri huo wa treni kutokea Dodoma. 
Aidha Sahani amesema ratiba ya huduma ya muda wa kuanzia Dodoma ni kwamba treni ya abiria itaondoka saa moja usiku kesho Jumanne na Ijumaa kwenda Kigoma, Mwanza na Mpanda ambako inatarajiwa kuwasili Mwanza saa 12 jioni siku ya Jumatano na Mpanda saa 12 jioni na Kigoma saa 12 jioni. 
"Treni kutoka Mpanda, Mwanza na Kigoma zitatoka huko siku za Jumapili na Alhamis tu. Mpanda inatoka saa moja asubuhi, Mwanza inatoka saa mbili asubuhi na Kigoma inatoka  saa1:30 asubuhi.Treni hizo zinafika Dodoma siku ya Jumatatu na Ijumaa saa 1:00 asubuhi, "amesema. 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi (Uendeshaji) Focus Sahani, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza mabadiliko ya muda ya Ratiba za usafiri wa Treni na kuharibika kwa miundombinu ya Reli eneo la Kilosa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini, ambapo usafiri huo kwa sasa utaanzia mkoani Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Usafirishaji, Shaaban Kiko. 
*****************************************
Wakati huohuo Sahani amesema treni pekee ya kutoka Tabora kwenda Mpanda itafanya safari zake siku za Jumanne, Alhamisi na Jumapili na itatoka Mpanda kurejea Tabora katika siku za Jumatatu, Jumatano na Jumamosi. 
"Itakuwa inaondoka Tabora saa  12 asubuhi na kuwasili Mpanda saa 12:32 na itaondoka Mpanda kurejea Tabora saa 1:00 asubuhi na kuwasili saa 12:32 jioni. Uongozi WA TRL bado unaendelea kusimamia kazi ya ukarabati wa eneo lililoharibika kati ya Kilosa na Gulwe, "amesema Sahani. 
Pia uongozi wa TRL umesema moja ya sababu inayochangia reli kuharibika kwa maji ya mvua inatokana baadhi ya wakulima kulima katika maeneo ya reli,hivyo wamehimiza walnaolima pembezoni kwa reli kuacha kwani madhara yake ni pamoja na kuharibu miundombinu ya reli. 
 Meneja wa Usalama wa Njia za reli Tanzania, Gukwi Michael (katikati) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari. 
Kaimu Meneja Masoko wa TRL, Iddi Mzugu, akifafanua jambo kuhusu uharibifu huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.