Habari za Punde

WACHEZAJI WA SIMBA WALIVYOPOKELEWA BANDARI YA DAR LEO

Baadhi ya washabiki wa Simba SC wakishangilia wakati wachezaji wa timu hiyo walipokuwa wakishuka katika Boti baada ya kuwasili Bandari ya Dar es Salaam wakitokea mjini Unguja baada ya kuondolewa katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Wachezaji wa Simba SC, Nicolaus Gyan na Asante Kwasi wakiwasili leo jijini Dar es Salaam kutokea visiwani Zanzibar mara baada ya kuondolewa katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A.
Mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi, Shiza Ramadhani Kichuya akikataa kuzungumza na waandishi wa habari bandarini hapo mara baada ya kuwasili leo Jijini Dar es salaam akitokea visiwani Zanzibar mara baada ya kuondolewa katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi .
Mshabiki wa Simba SC, Willium Mazoba akizungumzia kutolewa kwa timu ya Simba katika michuano ya Mapinduzi Cup Zanzibar Picha na Agness Francis

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.