Habari za Punde

WANAWAKE KUANZA KUUMANA FEBRUARI 24 LIGI YA SERENGETI PREMIER LITE

LIGI  ya Wanawake ya Serengeti Premier Lite hatua ya nane bora inatarajia kuanza kutimua vumbi Februari 24, 2018 kwenye viwanja vine.
Mchezo kati ya Kigoma FC na Simba Queens utakaochezwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika ndio utakuwa mchezo rasmi wa ufunguzi.
Mechi nyingine zitakazochezwa katika siku hiyo ya ufunguzi ni Panama watakaokuwa nyumbani Uwanja wa Samora kucheza na Evergreen,JKT Queens wakicheza dhidi ya Alliance kwenye uwanja wa Mbweni.
Mechi nyingine ni ile nitakayowakutanisha Baobab na Mlandizi Queens utakaochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kabla ya kufika kwenye hatua hiyo,ligi hiyo inayodhaminiwa na bia ya Serengeti Premier Lite kinywaji murua na chenye ubora wa juu ilianzia kwenye hatua ya makundi ikichezwa kwenye Kituo cha Dar Es Salaam kilichotumia Uwanja wa Karume na Kituo cha Arusha kilichotumia Uwanja wa General Tyre.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.