Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE AWAHASA WATANZANIA KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akiwasisitiza watanzania kuendelea kumwombea Mheshimiwa Rais kama jinsi amekuwa akiwaomba mara kwa mara katika mkutano wa maombi ya kuombea Taifa la Tanzania uliyoandaliwa na kanisa la Abundant Blessings Center jana jijini Dar es Salaam,aliyeketi kushoto ni Askofu wa Kanisa hilo Flaston Ndabila.
Askofu David Mwansoka wa Kanisa la Abundant akiongoza maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania kwa watu waliyojitokeza kushiriki  mkutano huo (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam wa pili kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe na wa kwanza kushoto Mkuu wa Wilaya Kibaha Asumpta Mshama wakifuatilia maombi hayo.
Askofu wa Kanisa la Abundant Flaston Ndabila akimweleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) namna kanisa hilo limekuwa na utaratibu wa kuombea Taifa katika mkutano wa kuliombea taifa la Tanzania na viongozi wake uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam,wa kwanza kushoto ni Askofu David Mwansoka wa Kanisa hilo.
Waumini wa Kanisa la Abundant wakiwa katika maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania yaliyokuwa yakiongozwa na Askofu David Mwansoka hayupo pichani jana jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alikuwa mgeni rasmi. Na Anitha Jonas – WHUSM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.