Habari za Punde

WAZIRI PALAMAGAMBA AHIMIZA MAHAKAMA KUTENDA HAKI

Waziri wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akipanda mti katika jengo jipya la mahakam ya mwanzo na Wilaya ya Kigamboni, baada ya kumaliza kuzindua mahakama hiyo mpya.
************************************
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ameitaka Mahakama kutenda Haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha Haki kutendeka.
Pia ameitaka kutoa fidia ipasayo, kukuza usuluhishi ipasavyo, kukuza usuluhishi baina ya watu husika katika migogoro na watoe haki bila kujali sababu za hali ya mtu kijamii ama kiuchumi
Waziri Kabudi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga maonesho ya Wiki ya Sheria ambayo kilele chake kinatarajiwa kufanyika kesho katika Viwanja vya Mahakama vya Chimala jijini. Kauli mbiu katika siku ya sheria mwaka huu inasema, Matumizi ya Tehama katika utoaji haki kwa wakati na kuzingatia maadili. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri Kabudi pia ameitaka Mahakama ipunguze kuchelewesha kesi bila sababu za msingi na iongeze kasi ya usikilizwaji wa Mashauri.
Ameongeza Wizara inathamini maonesho ya siku ya sheria na maendeleo yanayofanywa na Mahakama katika kuendeleza kuboresha mfumo wa sheria na kwamba Mahakama imekuwa ya kwanza kubadilika katika sekta ya sheria. Hivyo Wizara itahakikisha maboresho ya mahakama yanafanikiwa.
Kabla ya ufungaji wa maonesho hayo, Waziri Kabudi pia amezindua Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni.
Akizindua jengo hilo la Mahakama lililogarimu zaidi ya Sh.milioni 500 Prof.Kabudi amesema, mkakati wa Mahakama hadi kufikia mwaka jana walikuwa wanahitaji Mahakama Kuu 19, Mahakama za Hakimu Mkazi 14, Mahakama za Wilaya 109, Mahakama za Mwanzo 3003 huku wakiwa na uhitaji mkubwa wa ukarabati wa mahakama nyingi nchini. 
Aliipongeza Mahakama kwa ubunifu, umakini na ufanisi waliouonesha kwa kufanya utafiti wa kutumia Moladi na ujenzi bora, imara na wenye gharama nafuu. Prof. Kabudi pia ameipongeza mahakama kwa kujenga majengo hayo katika wilaya mpya, hasa Kigamboni na amewataka kutafuta viwanja zaidi ili jitihada za kuongeza mahakama Kigamboni zifanyike kwa kuwa ipo moja tu.
Pia ameshauri wananchi wa Kigamboni kuhakikisha wanajaribu kutafuta usuluhishi nje ya Mahakama kwa matatizo yanayowezekana na ikishindikana ndiyo wapeleke mahakamani. 
"Serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya Mahakama kila mwaka ili kuboresha huduma...nitoe rai kwa watumishi na watumiaji mtunze miundombinu, serikali imetumia fedha gharama nyingi muilinde na kuitunza,"amesema. 
Amebainisha mfumo wa Mahakama wa Tehama utapunguza gharama kwa kuwa utasaidia kesi kuendeshwa wakati shahidi akiwa eneo lingine na hata mtu kutumia simu ya kiganjani kupata taarifa za mahakama, kufungua kesi ama kulipa.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omary Othmani Makungu amefurahi nakuahidi kutumia elimu aliyoipata ili kujenga jengo kama hilo kwa gharama nafuu kwani wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika ujenzi wa mahakama Zanzibar.
Katika Wiki hii ya Sheria Mahakama amezindua majengo mapya katika mahakama za Bagamoyo, Kawe, Mkuranga, Kigamboni na Kituo cha Mafunzo Kisutu.
Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Pamalagamba Kabudi akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa Mahakama wakati wa uzinduzi mahakama ya mwanzo na Wilaya ya Kigamboni, kulia kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania, Ferdnandi Wambari na kulia kwake ni Jaji Mkuu Kuu Zanzibar Omary, Othaman Makungu.
Waziri wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa mahakama nchini Tanzania na Zanzibar

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.