Habari za Punde

BRIGHT AIFAGILIA 'SINA' KUMPAISHA KIMTINDO

Na Amina Kasheba, Dar
MSANII  wa muziki wa kizazi kipya nchini 'Bongo Flava', Rashidi  Said, ‘Bright’ amekamilisha kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Sina.
Wimbo huo unaoendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na mitandao ya kijamii, ameuachia mwanzoni mwezi uliopita.
Akizungumza na mtandao huu, Bright, ameweka wazi 
sababu za kupendwa na mashabiki wa muziki Bongo Flava, 
na wimbo wake huo kufanya vizuri kwa kipindi cha muda mfupi kuwa hasa ni maudhui ya wimbo wenyewe ukilinganisha na nyingine zilizotoka sambamba na wimbo huo.
“Nimefurahi kuona nazidi kupiga hatua katika kazi yangu ya usanii kupitia muziki wa kizazi kipya kwani naona ni jinsi gani muziki unavyonibadilisha na kunipa upeo hamu ya kuzidi kuwafurahisha mashabiki zangu kwa kuwapa zawadi ya nyimbo zisizowachosha,
Kwa hakika kati mafanikio yangu katika muziki basi wimbo huu wa Sina umenipa mafanikio ya haraka ambayo sikuyategemea”alisema Bright.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.