Habari za Punde

BRITISH COUNCIL YAWANOA WALIMU WA MSINGI NA SEKONDARI DAR NA PWANI

Na Amina Kasheba, Dar
WAKUU wa shule za sekondari na msingi za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, wamepewa mafunzo ya kuongeza ujuzi katika ufundishaji na ufaulu wa masomo kwa wanafunzi, walimu wa chini yao.
Mafunzo hayo ya siku tatu yametolewa na British Council chini ya mradi wa ‘Connecting classroom’, ili kufikia lengo la kuwajengea uwezo walimu kwa ajili ya kuongeza ufaulu katika shule zao na jinzi ya kuishi na wanafunzi.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Mkufunzi wa mradi huo, Edwin Steevern, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa walimu ni kuwaongezea ujuzi katika kazi zao za ufundishaji na kuongeza mbinu mbalimbali za kuboresha ufaulu mzuri wa kitaaluma.
“Tunawafundisha walimu kwa dhumuni la kuwaongezea ujuzi zaidi wa ufundishaji pamoja na kuishi na wanafunzi mashuleni, kwasababu walimu wanakumbana na matatizo mengi katika kazi zao na wanawafundisha wanafunzi ambao wametoka katika familia tofauti,” amesema Edwin.
Akielezea kuhusu mafunzo hayo Ofisa elimu Msingi wa Manispaa ya Kinondoni, Kiduma Mageni, amesema mafunzo hayo ni mazuri kwa walimu wao katika kuboresha sekta ya elimu na hasa ukizingatia lengo la mafunzo hayo.
Kiduma aliongeza kuwa wanaimani kupitia mafunzo hayo ya mradi wa ‘Conneting classroom’ yataleta mabadiliko makubwa kwa walimu japo ni ya muda mfupi.
“Mafunzo yalikuwa ya muda mfupi, lakini tunawashukuru British Council kwa kuwaongezea ujuzi wakuu wetu wa shule kwani na walimu wetu wameongeza ujuzi wa baadhi ya mambo’’ amesema
Kwa upande wake Meneja wa mradi huo, Ephraim Kapunga, amesema mafunzo hayo yalianza mwaka 2015 kwa kuzunguka sehemu mbalimbali nchini kwa nia ya kutoa elimu kwa kushirikiana na maofisa wa elimu wa shule za msingi na sekondari.
Na kuongeza kuwa mbali na mkoa wa Dar es Salaam, tayari wametoa mafunzo kwa wakuu wa shule za msingi na sekondari katika mikoa ya Dodoma, Tabora na Manyara.
“Malengo yetu ni kufika mikoa yote Tanzania,” alisema Kapinga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.