Habari za Punde

KARANI ALIPA MILIONI 100 KUKWEPA ADHABU YA KIFUNGO CHA MIAKA 3 JELA

Na Mwandishi Wetu, Dar
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Karani wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA, Winfred Businge (33) kulipa faini ya Sh milioni 100 ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela. Baada ya kupatikana na hatia ya tuhuma za kushindwa kutolea maelzo USD milioni moja kwa afisa forodha.
Businge ambaye ni raia wa Uganda alifanikiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha cha Sh milioni 100 na kukwepa adhabu hiyo ya kifungo.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa, kukubali kosa.
Katika hati ya mashtaka, ilidaiwa Desemba 11, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ndani ya jiji la Dar es Salaam Businhe alikutwa ameingia nchini na USD milioni 100 ambazo ni sawa na sh. Bilioni 2 fedha ambazo alishindwa kuzitolea maelezo kwa wakala wa forodha.
Kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Wakili wa serikali mwandamizi, Awamu Mbagwa, kwa upande wa utetezi alikuwa akiwakilishwa na Wakili Hudson Ndusyepo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.