Habari za Punde

MAANDALIZI YA UCHAGUZI JIMBO LA SIHA YAMEKAMILIKA

Zikiwa zimebakia siku tatu kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mdogo katika Majimbo 2 na Kata 8 za Tanzania Bara, maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Siha na Udiwani katika Kata 3 za jimbo hilo lililopo mkoani Kilimanjaro yamekamilika.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo  Bwana VALERIAN MARGWE JUWAL amesema vifaa vyote kutoka Tume Makao Makuu kwa ajili ya Uchaguzi huo tayari vimepokelewa na kwamba Mafunzo kwa Watendaji wa Uchaguzi yanaendelea.
Akizungumzia kuhusu kampeni zinazoendelea kwa Vyama vinavyoshiriki Uchaguzi huo Bwana JUWAL amesema kumekuwepo na vitendo vinavyokiuka Maadili ya Uchaguzi ingawa kamati ya Maadili imekuwa ikichukua hatua kwa mujibu wa taratibu.
Ametaja baadhi ya vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ambavyo vimewasilishwa katika Kamati ya Maadili kuwa ni pamoja na baadhi ya wanachama wa Vyama vya siasa kufanya Maandamano baada ya mikutano, baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Vyama hivyo kutoa kauli za vitisho na lugha za maudhi dhidi ya Vyama vingine.
Msimammizi huyo wa Uchaguzi ambaye amewataka wakazi wa Jimbo la Uchaguzi la Siha kujitokeza siku ya Uchaguzi ili kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wao na kutahadharisha watu au kikundi chochote cha watu watakaojaribu kuvuruga Uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.